ASKOFU GWAJIMA ASHTAKIWA BUNGENI

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mhe. Job Ndugai (Mb) ameamuru Mheshimiwa Josephat Mathias Gwajima na Mbunge Jerry Slaa wapelekwe mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge ili kujibu tuhuma mbalimbali ikiwemo kusema uongo na kushusha hadhi na heshima ya Bunge. Askofu Gwajima na Jerry Slaa wanatakiwa kufika mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge Jumatatu tarehe 23 Agosti, 2021 .